Haya tena watanza wenye nia njema tunakutana kwa mara nyingine katika uwanja wetu wa mazingira na maliasili. Samahani kwa kuwa kimya kwa muda mrefu, ila tupo pamoja siku zote. Mada yetu ya leo kwa kweli ni hot issue kwa sasa hapa duniani. Si mnakumbuka juzi juzi tu kulikua na kikao juu mabadiliko ya tabia nchi kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa? Nikwambieni kitu cha kuchekesha, msafara wa Tanzania unaambiwa ulikua mkubwa kuliko hata wa China na Marekani, ilhali hizo nchi ndio zinazoshutumiwa kwa kusababisha mabadiliko haya!!
Kwa mujibu wa "wataalamu" wa sayansi ya tabia nchi, kasi ya mabadiliko kwa sasa ni ya kutisha kutokana na shughuli za wanadamu, na inasemekana joto linaongezeka kwa kasi ambayo haijawahi kutokea hapo awali. Mdahalo wa ili suala kwa kweli wadau ni mkubwa mno. Kuna wanaosema kua "wataalamu" hawa wanamanipulate na kucook data ili ionekana kua kuna tatizo la kutisha wakati tatizo si la kutisha sana; na hawa wanaamini kua mabadiliko haya hayasababishwi na wanaadamu, bali ni mifumo tu ya ulimwengu na jua (solar system). Wanasema wanaadamu wanapandikiziwa mzigo husio wao, wanauliza mbona hata wakati wa Yusuf kule Misri, kuliktokea baa la ukame na njaa kwa miaka saba? Je, hiyo nayo utaiitaje? Pia wanauliza mbona kulikua na kipindi kilichoitwa ice age? Na kilitoweka tu mara moja, na baadhi ya masalia ya kipindi hiko ni mlima Kilimakyaro. Kiujumla wanasisitiza kua, mabadiliko ya tabia nchi yalikuwepo siku zote na yataendelea kuwepo, hisiwe leo wana wa Adamu wakabebeshwa mzigo husio wao.
Kwa upande mwingine, kuna hawa ambao wanasisitiza kuwa, yanatokea sasa hivi yote yanasababishwa na wana wa Adamu. Hapa kuna umoja wa mataifa, na mashirika yake kama, mapngo wa mazingira (UNEP), mtandao wa jumuiko la serakali la mabadiliko ya tabia nchi (IPCC), na sasa nyingi ya nchi maskini nazo zinaanza kushabikia huu wimbo kwa sababu ya fursa za mishiko zinazokuja na nyimbo hii. Hawa wanasema binadamu ndio chanzo, na ndio anapaswa kuwajibika katika kupunguza na kukabiliana na tatizo ili. Sawa, je, Marekani na China si ndio vyanzo katika hili? Je, wanafanya nini zaidi ya kusukuma majukumu kwa nchi maskini kwa mtindo wa kuleta pesa chafu (nasikia wanafanya money laundering) kupitia mikakati yao kama vile REDD (Reduced Emission through Decreased Forest Degradation), na pia biashara ya gesi mkaa (carbondioxide)?!!?!?! Hii biashara ya gesi mkaa tena imeng'ang'aniwa sana nchi Marekani and Norway, kwa sababu, kupitia biashara hii wataweza kutoa zaidi gesi mkaa ilhali kuna nchi maskini ambazo zipo tayari kuuza viwango vyao vya utowaji wa gesi hiyo, ili kupata faida. Je, hapo Marekani na wenzake wanawajibika au wanatuwajibisha?!??
Jamani, kwa leo naomba niishe hapa tu. Ila haya ni maoni yangu, nakaribisha pia michango yenu wadau. Asanteni.